UTAMBULISHO WETU

Holiness Gospelers Assembly (HOGOA) ni Huduma yaki injilisti yaani kusanyiko la Wahubiri Watakatifu, iliyoanzishwa na Mchungaji Conrad Julias Lusale. Lengo kuu ni kuhubiri neno la Mungu kwa watu wote na kuwafundishs waishi maisha matakatifu kama Injili ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo inavyofundisha. Tunatekeleza agizo lake katika Injili ya Mathayo 28
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu;

20 na kuwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi. na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Tunakusudia Huduma hii ifike kwa watu wa rangi zote, makabila, lugha na mataifa yote. Mfumo wa uinjilisti utafanyika katika nyanja mbalimbali, zikiwemo mtandao, kwa njia ya vipeperushi, kupitia vyombo vya habari, mahubiri, mikutano ya hadhara na njia nyinginezo zitakazo onekana zinakubalika katika maeneo husika.

Kwa vipindi vya mwanzo, tutatumia rugha kuu mbili yaani Kingereza na Kiswahili.
Napenda kutumia nafasi hii Kuku alika na wewe tushirikiane pamoja kumshambulia shetani. na Mungu atakubariki.